Matthew 4:1-6

Kujaribiwa Kwa Isa

(Marko 1:12-13; Luka 4:1-13)

1 aKisha Isa akaongozwa na Roho Mtakatifu kwenda nyikani ili akajaribiwe na ibilisi. 2 bBaada ya kufunga siku arobaini usiku na mchana, hatimaye akaona njaa. 3 cMjaribu akamjia na kumwambia, “Ikiwa wewe ndiye Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”

4 dLakini Isa akajibu, “Imeandikwa: ‘Mtu haishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.’ ”

5 eNdipo ibilisi akamchukua Isa mpaka mji mtakatifu na kumweka juu ya mnara mrefu wa Hekalu, 6 fakamwambia, “Kama wewe ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini. Kwa kuwa imeandikwa: “ ‘Atakuagizia malaika zake,
nao watakuchukua mikononi mwao
ili usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.’ ”

Copyright information for SwhKC